Barsen
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Barsen wa Edessa (pia: Barses, Barsus, Barsas; alifariki Filo au Thenon, Misri, Machi 378) alikuwa askofu wa Carre, halafu askofu mkuu wa Edessa, leo Urfa, nchini Uturuki, kuanzia mwaka 361, baada ya kuishi miaka mingi kama mkaapweke.
Mwaka 373 alifukuzwa jimboni kutokana na dhuluma ya kaisari Valens aliyetetea Uario [1]. Kwanza alipelekwa katika kisiwa cha Arwad, huko Foinike (leo nchini Syria), halafu el-Bahnasa, Misri, hatimaye mbali zaidi na watu karibu na Libya.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads