Barua za Shaaban Robert 1931-1958

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Barua za Shaaban Robert 1931-1958 ni mkusanyo wa barua zipatazo kama mia moja ambazo zilihifadhiwa na Yusuph Ulenge kwa zaidi ya miaka sitini kabla ya kuja kukabidhiwa kwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili mnamo mwaka 1993 wakati wataalamu toka katika taasisi hiyo walipokuwa wakifanya utafiti. [1]

Kitabu hiki ni zawadi nzuri kwa waandishi na watunzi wa mashairi kwa sababu kimeelezea mambo ambayo yalikuwa hayafahamiki na wengi kuhusu Shaaban Robert na ukoo wake [2]

Katika kitabu hiki, kimedhihirisha pia uwezo mwingine wa Shaaban Robert wa kuzungumza na kuandika lugha ya kigeni ya Kiingereza, jambo ambalo wengi walikuwa hawafahamu kama mtaalamu huyo wa Kiswahili alikuwa anafahamu hadi lugha za kigeni na hata kusoma kwa njia ya posta.

Ndani ya kitabu hiki, msomaji ataweza kufahamu zaidi kuhusu imani aliyokuwa nayo Shaaban Robert katika suala la elimu hadi kumsisitizia ndugu yake Yusuoh Ulenge asimame katika elimu.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads