Bata-maji

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bata-maji
Remove ads
Remove ads

Mabata-maji ni ndege wakubwa wa maji wa jenasi Cygnus katika familia ya Anatidae. Wanaainishwa katika nusufamilia Anserinae pamoja na mabata bukini. Mabata-maji ni ndege wakubwa kabisa wa familia yao wenye shingo ndefu na domo pana. Spishi za nusudunia ya kaskazini zina rangi nyeupe tu, lakini spishi za nusudunia ya kusini ni nyeupe na nyeusi. Hula mimea ya maji hasa lakini manyasi mafupi na wadudu pia. Tago lao limejengwa kwa matete na mimea ya maji juu ya nchi kavu lakini karibu sana ya maji.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Ndege hawa huzaana kwa kanda za kaskazini na kusini za dunia. Wakati wa majira ya baridi au ukavu huhama kanda za moto zaidi au ambapo mvua unanyesha. Spishi kadha, hususa Bata-maji Domo-fundo na Bata-maji Mweusi, zimewasilishwa nje ya eneo lao la usambazaji, k.m. Afrika ya Kusini.

Remove ads

Spishi za Afrika

  • Cygnus atratus, Bata-maji Mweusi (Black Swan) imewasilishwa katika Afrika ya Kusini
  • Cygnus olor, Bata-maji Domo-fundo (Mute Swan) inapatikana kwa kawaida katika Afrika ya Kaskazini, lakini imewasilishwa katika Afrika ya Kusini

Spishi za mabara mengine

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads