Ben Pol
Mtanzania, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo. From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bernard Michael Paul Mnyang’anga (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ben Pol; amezaliwa 8 Septemba 1989) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya na mwigizaji kutoka nchini Tanzania. Hasa anaimba muziki wa R&B.
Ben Pol alianza kujulikana mnamo mwaka 2010 baada ya kutoa kibao cha "Nikikupata" ambacho kiliweza kumtambulisha katika ulimwengu wa Bongo Flava. Kwa asili Ben ni mtu wa Dodoma[1], tena anajisifu kama mtu kutoka kanda ya kati.
Remove ads
Nyimbo
Baadaye akaja kutamba zaidi na vibao kama vile
- Samboira
- Moyo Mashine
- Jikubali
- Phone
- Nikikupata
- Namba One Fan
- TATU
- Sophia
Upande wa filamu, amepata kucheza katika filamu ya Sunshine na baadhi tu ya filamu zilizokuwa chini ya MFDI Tanzania na kuongozwa na Karabani.[2]
Tuzo
Ameshinda tuzo za mziki Tanzania (KTMA) Kwa miaka mitatu mfululizo kudhibitisha ubora wake katika muziki wa R&B.
- 2012
- 2013
- 2014
Ameshinda tuzo za www.mdundo.com
- 2016
Tuzo za hipipo Uganda
- 'Muzuki' wimbo bora wa Afrika Mashariki
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads