Benazir Bhutto
Waziri mkuu wa 11 na 13 wa Pakistan (1953-2007) From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Benazir Bhutto (21 Juni 1953 - 27 Desemba 2007) alikuwa mwanasiasa kutoka nchini Pakistan. Alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa na kuongoza nchi ya Kiislamu. Pia alishawahi kuchaguliwa kuwa kama Waziri Mkuu wa Pakistani mara mbili kuanzia 1988 hadi 1990 na 1993 hadi 1996. Alikaa ugenini 1999 bis 2007 kutokana na udikteta ya kijeshi na baada ya kurudi kwake aliuawa wiki mbili kabla ya uchaguzi ya kitaifa alimogombea.

Remove ads
Shughuli za Kiserikali (kwa ufupi)
Benazir Bhutto alikuwa binti wa waziri mkuu wa Pakistan Zulfikar Ali Bhutto aliyepinduliwa na jeshi mwaka 1977 na kunyongwa 1979. Benazir alienda kukaa ugenini akawa kiongozi wa chama cha babake na baada ya kurudi alishinda uchaguzi wa mwaka 1988. Aliapishwa kama waziri mkuu kwa mara kwanza tar. 2 desemba 1988, lakini aliondolewa madarakani baada ya miezi 20 kwa kashfa ya vitendo vya rushwa, wakati nchi iko chini ya rais Ghulam Ishaq Khan. Ilivyofika mwaka wa 1993 Bhutto akachaguliwa tena, lakini aliondoshwa madarakani tena kwa kashfa zilezile za awali. Lakini sasa amechaguliwa tena na Rais Farooq Leghari na hakuondoka tena maradarakani hadi hapo kifo chake kilipomfika.
Remove ads
Kuawa kwake
Mnamo tar. 27 Desemba ya mwaka 2007, Benazir Bhutto aliuawa pindi alipokuwa akiingia ndani ya gari lake akiwa anatokea katika mkutano wa kisiasa wa Chama cha kisiasa cha Pakistan People Party (PPP), mjini Rawalpindi, Pakistan. [1] Alipigwa risasi ya shingo na ya kifua kabla ya kufyatua bomu la kuvaa mwilini. Tukio hili lilisababisha kuuawa kwa watu wapatao 30 na kujeruhi wengine kibao. Anaitwa Shaheed-e-Jaumhuriat (Shahidi wa Demokrasia) na washabiki wake.
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads