Benwadi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Benwadi wa Hildesheim (jina asili: Bernward; 960 – 20 Novemba 1022) alikuwa askofu wa Hildesheim nchini Ujerumani kuanzia tarehe 15 Januari 993 hadi kifo chake[1] [2].


Alilinda kundi lake dhidi ya maadui, aliendesha sinodi nyingi ili kurudisha nidhamu ya wakleri na alistawisha umonaki[3].
Benwadi aliagiza ujenzi wa kanisa kubwa la Mt. Mikaeli kwa mtindo wa Kiroma na pia kutengenezwa kwa milango ya shaba kwa kanisa kuu la Hildesheim; yote mawili yametambuliwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia[4].
Papa Selestini III alimtangaza mtakatifu tarehe 19 Desemba 1192.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tarehe 20 Novemba[5].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads