Big Pun
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Christopher Rios (anafahamika zaidi kwa jina la kisanii Big Punisher au Big Pun: 9 Novemba 1971 - 7 Februari 2000) alikuwa msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Huyu alikuwa Mpuerto Rico-Mwamerika na alianza kupata umaarufu mwanzoni kabisa mwa miaka ya 1990 akiwa mjini The Bronx.
Huyu ni mmoja kati ya waanzilishi wa kundi la muziki wa hop hop la Terror Squad. Alianza kuonekana kwa mara ya kwanza katika albamu ya The Beatnuts, kwenye nyimbo ya "Off the Books", na katika albamu ya pili ya Fat Joe ya Jealous One's Envy, tena kwenye wimbo wa "Watch Out", alioimba kwa mara ya kwanza akiwa kama msanii wa kujitegemea kufanyakazi na studio ya Loud Records.
Juhudi zake katika muziki zilikujakwisha katika mwaka wa 2000 akiwa na umri wa miaka 28. Big Pun alikufa kwa shinikizo la moyo. Bwana huyu ameacha mke, Liza Rios, na watoto watatu. Anakadiriwa kuwa alifariki akiwa na uzito wa paundi 700 ambazo ni sawa na kilogramu 300. Kila kitu kuanzia kuoga na kuvaa hadi viatu, alikuwa akisaidiwa kufanya shauri ya uzito mkubwa aliokuwa nao.
Remove ads
Diskografia
Albamu za Studio
Akiwa kama mwanachama wa Terror Squad
- 1999: Terror Squad
- 2004: True Story ("Bring 'Em Back" akiwa na Fat Joe na Big L)
Remove ads
Single
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads