Terror Squad
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kwa matumizi mengine, angalia Terror Squad (maana)
Remove ads
Terror Squad ni kundi la muziki wa hip hop na pia studio kutoka mjini Bronx, New York, ambalo lilianzishwa mnamo mwaka 1998 kwa kupitia kibao kimoja mashuhuri kinachotoka katika albamu ya Don Cartagena ya mwimbaji kiongozi wa kundi hilo Fat Joe.
Walitoa albamu yao ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Terror Squad, kunako 1999, ikiwa imeambatana na kibao chao cha kwanza kilichokwenda kwa jina la "Whatcha Gon' Do", ambacho kiliimbwa zaidi na Big Punisher, ambaye alifariki dunia kwa tatizo la ugonjwa moyo manmo mwa 2000. Baada ya kifo cha Big Pun, washikaji zake wa toka kitambo Bw. Cuban Link na Triple Seis, wakajitoa katika kundi na badala yao nafasi hizo zikawa nimeshikiliwa na Remy Martin na Tony Sunshine.
Kama jinsi vile kundi lilivyo simama kwa kufuatia kifo cha Big Pun, wanachama wengi wa kundi hilo wakaangukia katika fumbo zito kwa kufuatia mafanikio makubwa alioyoyapata rapa mwenzao Fat Joe, akiwa kama msanii wa kujitegea na kuwashinda hata wale wenzake.
Kundi lilirudi tena ulingoni na wakafanikiwa kutoa albamu yao ya pili iliyokwenda kwa jina la True Story, mnamo mwaka wa 2004. Albamu ilibeba byimbo maarufu ya "Lean Back," ambayo ilitayarishwa na Scott Storch, na kuweza kushika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard Hot 100 bora na nafasi ya 24 katika UK.[1]
Remove ads
Muziki
Album
- Terror Squad - The Album
- Imetolewa: 21 Septemba 1999
- Chati iliyoshika: #22 US
- Maelezo ya RIAA: -
- Single: Whatcha Gon Do
- True Story
- Imetolewa: 27 Julai 2004
- Chati iliyoshika: #24 US
- Maelezo ya RIAA: Gold
- Single: Lean Back, Take Me Home, Yeah Yeah Yeah
- New Story
- Imepangiliwa:2008
- Chati iliyoshika: HKN
- Maelezo ya RIAA:
- Single: Hamna
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads