Bikira Maria wa Mlima Karmeli

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bikira Maria wa Mlima Karmeli
Remove ads

Bikira Maria wa Mlima Karmeli ni jina linalopewa Bikira Maria kama msimamizi wa Wakarmeli. Wa kwanza wao walikuwa wakaapweke walioishi mwishoni mwa karne ya 12 na mwanzoni mwa karne ya 13 katika Nchi Takatifu juu ya Mlima Karmeli, ambapo zamani Nabii Eliya alirudisha Waisraeli kumuabudu Mungu aliye hai [1].

Thumb
Bibi Yetu wa Mlima Karmeli, mchoro wa Pietro Novelli, 1641.

Katikati ya makazi yao walijenga kikanisa kwa heshima ya Bikira Maria, msimamizi wao.

Tangu karne ya 15 watu wamemheshimu kwa jina hilo hasa kwa kuvaa skapulari ya kahawia inayosemekana Maria alimpa Mkarmeli Simoni Stock (1165-1265).

Kumbukumbu katika liturujia inafanyika tarehe 16 Julai.[2][3][4][3]

Remove ads

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads