Bolivia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bolivia
Remove ads

Bolivia (jina linatokana na shujaa Simon Bolivar) ni nchi isiyo na mwambao wa bahari katika Amerika Kusini.

Ukweli wa haraka


Thumb
Ramani ya Bolivia
Thumb
Mji wa La Paz
Thumb
Uyuni

Imepakana na Brazil, Paraguay, Argentina, Chile na Peru.

Remove ads

Jiografia

Nchi inakatwa na safu mbili za milima ya Andes zenye kimo hadi mita 6500 juu ya UB.

Nyanda za juu (kwa Kihispania: "Altiplano") zinakaliwa na wakazi wengi (80%) ziko kwenye kimo cha mita 3.000 hadi 4.000. Altiplano ni takriban theluthi moja ya eneo la nchi; sehemu nyingi ni tambarare ya "llanos" ambayo ni nchi ya chini yenye joto ambayo ina sehemu mbili: savana kavu za Gran Chaco na misitu minene ya beseni ya Amazonas.

Ziwa la Titicaca liko kwenye Altiplano.

Bolivia ni kati ya nchi maskini zaidi za Amerika Kusini.

Remove ads

Watu

Tofauti na nchi nyingine za bara hilo, wakazi asilia (Waindio) ni sehemu kubwa ya wananchi (55%), wakifuatwa na machotara (30%) na watu wenye asili ya Ulaya (15%).

Lugha rasmi ziko 37, kuanzia Kihispania na lugha nyingi asilia.

Upande wa dini, Kanisa Katoliki linaongoza (78%), likifuatwa na Uprotestanti (19%).

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads