CECAFA

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Council for East and Central Africa Football Associations (kwa Kiswahili Baraza la Mashirikisho ya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati, kifupisho rasmi CECAFA) ni shirikisho la mataifa yanayoshiriki mchezo wa mpira wa miguu hasa katika Afrika Mashariki na sehemu za Afrika ya Kati. Kama mwanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), CECAFA ni shirikisho la mpira wa miguu lenye historia ndefu zaidi katika eneo la kikanda barani Afrika.

Remove ads

Historia

CECAFA ilianzishwa kwa njia isiyo rasmi mnamo mwaka wa 1927. Mashindano haya yalidhaminiwa na kampuni kubwa ya kutengeneza sabuni yenye makao makuu jijini Nairobi, Gossage, iliyo milikiwa na Lever Brothers wa Uingereza. Kuanzishwa kwake mara nyingi kunahusishwa visivyo na William Gossage, mwanzilishi wa kampuni ya Gossage. Hata hivyo, alifariki miaka 50 kabla ya CECAFA kuanzishwa.[1]

Michuano hii ilijulikana kama Gossage Cup hadi katikati ya miaka ya sitini, ambapo ikapewa jina jipya la East African Challenge Cup. Ilihusisha timu 12 pekee.

Ofisi kuu za CECAFA zipo Nairobi, Kenya. Mashindano ya kwanza yalikuwa kati ya timu za Kenya na Uganda, ambapo Kenya ilishinda michezo miwili kwa jumla ya magoli 3-1.

Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads