Cadimi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Cadimi (pia: Kadimi - kupitia Kilatini "Cadmium" kutoka Kigiriki καδμεία kadmeia iliyotaja mitapo yenye cadimi kwa heshima ya mungu wa Kigiriki Κάδμος Kadmos) ni elementi na metali haba duniani. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Cd na namba atomia 48 katika mfumo radidia.
Remove ads
Tabia na matumizi
Cadimi ni metali laini yenye rangi nyeupe-buluu. Hufanana mara nyingi na tabia za zinki lakini humenyuka kwa urahisi zaidi. Cadimi yenyewe na kampaundi zake huwa sumu na kusababisha kansa.
Matumizi yake ni hasa katika betri na viungo vya rangi. Kwa teknolojia ya kinyuklia hutumiwa kama kinga dhidi ya nyutroni katika matanuri ya nyuklia.
Nondo za Cadimi zilitumiwa na Enrico Fermi mwaka 1942 katika tanuri nyuklia ya kwanza kwa kusudi la kutawala mmenyuko mfulizo wa nyuklia. Nondo hizo zilisukumwa kati ya nondo za urani na kupunguza mwendo wa nyutroni kati ya nondo za urani.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cadimi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads