Kaliforni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kaliforni (Californium) ni elementi ya kikemia yenye alama Cf na namba atomia 98. Ni metali nururifu iliyopangwa katika kundi la aktinidi kwenye jedwali la elementi. Isotopi kadhaa huwa na nusumaisha ya miaka mamia hadi 13,000 lakini isotopi nyingi hudumu dakika chache tu. [1]

Kaliforni haipatikani kiasili, ni elementi sintetiki. Ilitengenezwa mara ya kwanza kwenye mwaka 1950 na wanasayansi katika maabara ya Chuo Kikuu cha Kalifornia mjini Berkeley na kupokea jina la jimbo hilo. Ilipatikana baada ya kufyatulia chembe alfa kwa atomi za Curi.
Kaliforni ni kati ya elementi sintetiki chache zinazotumiwa lakini kwa tahadhari kubwa kwa sababu ya unururifu wake ulio hatari kiafya. Kaliforni hutumiwa hasa kama chanzo cha nyutroni
- katika tiba ya saratani [2]
- katika tasnia ya uchunguzi wa vifaa na dutu mbalimbali [3]
- kwa kupima unyevu katika uchimbaji wa petroliamu (kutambua tofauti kati ya maji na matabaka yanayozaa mafuta)
- kwa kutambua vilipukaji vilivyofichwa
- kama chanzo cha kuwasha mchakato ndani ya tanuri nyuklia [4]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads