Chad (ziwa)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Chad (ziwa)
Remove ads

Ziwa Chad ni ziwa kubwa lisilo na njia ya kutoka lenye kina kidogo katika kanda la Sahel, kando ya jangwa kubwa la Sahara, kule ambako nchi za Chad, Kamerun, Niger na Nigeria zinapopakana, hivi kwamba eneo lake limegawanywa kati ya nchi hizo. Ziwa Chad lina umuhimu mkubwa kwa uchumi wa watu milioni 68 katika nchi hizo nne.

Ukweli wa haraka Ziwa Chad ...

Beseni lake ni beseni kubwa le bara la Afrika. Hata hivyo, eneo la uso wake limebadilika katika mwendo wa karne zilizopita kutegemeana na kiasi cha maji lilichopokea na kiwango cha uvukizaji na matumizi ya maji yake.

Ziwa Chad lilipungua kwa asilimia 98 baina ya miaka 1963 na 1998 lakini picha za satelaiti za ESA zimeonyesha ya kwamba baada ya hapo limepanuka tena kiasi. [1]

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads