Chad
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Chad, kirasmi Jamhuri ya Chad (pia: Chadi), ni nchi huru iliyoko Afrika ya Kati. Imepakana na Libya, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamerun, Nigeria na Niger. Mji mkuu ni Ndjamena.
Remove ads
Remove ads
Jiografia
Sehemu kubwa ya eneo lake ni jangwa na nchi yabisi. Kusini kuna kanda lenye hali ya hewa ya kitropiki, lakini ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo ni asilimia 3 tu za eneo lake lote .
Kaskazini kuna milima ya Tibesti.
Katikati liko beseni la ziwa Chad lililokuwa kati ya maziwa makubwa kabisa duniani lakini limepungua sana, hasa mwishoni mwa karne ya 20.
Historia
Katika milenia ya 7 KK kulikuwa na watu wengi sana katika beseni hiyo.
Katika historia kabla ya ukoloni watu wa kaskazini waliwafanyia vita watu wa kusini na kuteka wafungwa kama watumwa. Hivyo hadi leo uhusiano kati ya kusini na kaskazini ya nchi ni mgumu.
Tangu mwaka 2003 petroli imekuwa inaongoza kati ya bidhaa zinazopelekwa nje ya nchi badala ya pamba.
Tangu mwaka huo Mgogoro wa Darfur nchini Sudan umevuka mpaka na kuvuruga Chad pia. Ikiwa kati ya nchi zinazoongoza duniani kwa ufukara na ufisadi, ilipata shida kupokea wakimbizi kwa mamia elfu.
Ingawa kulikuwa na vyama vingi vya siasa na mapigano ya kisiasa pamoja na majaribio ya mapinduzi, mamlaka ilibaki imara mikononi mwa Rais Déby na chama chake, Patriotic Salvation Movement, hadi alipouawa mwaka 2021.
Remove ads
Watu

Wakazi walikuwa 15,500,000 mwaka 2018.
Jinsi ilivyo katika nchi mbalimbali za kanda la Sahel kuna aina mbili za wakazi ndani yake:
- Kaskazini wako hasa watu walioathiriwa sana na utamaduni wa Uislamu (55% za wakazi wote[5], wengi wakiwa Wasuni[6]). Mifano ni Waarabu (12.3%), Wafulbe, Wahaussa, Wazaghawa na wengineo. Wengi wao walikuwa wafugaji na sehemu ya makabila inaendelea hadi leo maisha ya kuhamahama.
- Kusini wako hasa watu wanaofuata Ukristo (41%, Wakatoliki wakiwa wengi kidogo kuliko Waprotestanti[7]) au dini asilia za Kiafrika (1%) kama Wasara (27.7%). Wengi wao hulima.
Kwa jumla leo kuna makabila zaidi ya 200 nchini, ambayo hutimia lugha na lahaja zaidi ya 100 (angalia orodha ya lugha hizo). Asili yao ni Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Afrika Magharibi na Afrika Kaskazini vilevile[8].
Lugha rasmi ni Kiarabu na Kifaransa.
Tazama pia
Marejeo
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads