Maafa ya Chernobyl

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Maafa ya Chernobyl yalikuwa maafa ya nyuklia yaliyotokea 26 Aprili 1986 katika tanuri la nyuklia la Chernobyl karibu na mji wa Pripyat, Ukraine. Wakati ule Ukraine ilikuwa jimbo la Umoja wa Kisovyeti. Kituo hicho kilikuwa karibu kilomita 110 kaskazini mwa mji mkuu, Kyiv.

Tukio hilo lilikuwa moja ya ajali mbaya zaidi katika historia ya nishati ya nyuklia. Jengo la tanuri halikuwa na zuio la mionzi na hivyo mnururisho wa nyuklia ulisambaa katika sehemu za magharibi mwa Umoja wa Kisovyeti, Ulaya ya Mashariki na Ulaya ya Kati, Skandinavia, Uingereza, na mashariki mwa Marekani . Maeneo makubwa ya Ukraine, Belarus na Urusi yalichafuliwa vibaya. Takriban 60% ya athari ya mionzi ilitua Belarus. [1] [2] Takriban watu 360,000 walipaswa kuhamia maeneo mengine.

Watu wengi waliteseka na athira ya mionzi na magonjwa ya muda mrefu kama saratani ya tezi. [3] [4]

Remove ads

Chanzo cha ajali

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads