Belarus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Belarus (kwa Kibelarus: Беларусь (Kisirili) au Byelarus (Kilatini); kwa Kirusi:Белоруссия ) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki inayopakana na Urusi, Ukraine, Poland, Lithuania na Latvia.
Remove ads

Mji mkuu ni Minsk na miji mingine ni pamoja na Brest, Grodno, Gomel, Mogilev na Vitebsk.
Idadi ya wakazi inapungua: ni watu 9,498,700 (2016).
Remove ads
Historia
Tazama pia: Historia ya Belarus
Belarus haikuwahi kuwa nchi ya pekee hadi karne ya 20. Maeneo yake yalikuwa chini ya himaya mbalimbali kama vile Poland, Lithuania na Urusi. Belarus ilikuwa kitengo cha Umoja wa Kisovyet tangu 1919/1922 hadi 1991.
Wakazi na utamaduni
Wakazi walio wengi ni Wabelarus (83.7%) ambao wanaongea ama Kibelarus au Kirusi ambavyo vyote viwili ni lugha rasmi. Lugha hizi mbili zina asili moja. Takriban 11% za wakazi ni Warusi.
Kuna pia vikundi vidogo vinavyotumia lugha za pekee kama vile Kipoland, Kiukraine, Kilatvia, Kilituanya na nyingine.
Walio wengi ni wafuasi wa Ukristo katika Makanisa ya Kiorthodoksi (48.3%) na katika Kanisa Katoliki (7.1%).
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads