Christina Milian

From Wikipedia, the free encyclopedia

Christina Milian
Remove ads

Christina Milian imeelekezwa hapa. Kwa albamu, tafadhali tembelea Christina Milian (albamu)

Ukweli wa haraka Maelezo ya awali, Jina la kuzaliwa ...

Christine Flores (amezaliwa 26 Septemba 1981) ni mtunzi, mwimbaji wa muziki wa pop na R&B, mtayarishaji, mnenguaji, na mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Christina Milian. Alizaliwa mjini Jersey City, New Jersey, halafu baadaye akahamia zake mjini Los Angeles. Akiwa na umri wa miaka ipatayo kumi na tatu, Milian akaanza kutamani kuwa mwigizaji.

Milian alipata kutoa albamu yake ya kwanza ya muziki iliyokwenda kwa jina lake mwenyewe, yaani Christina Milian, na wimbo maarufu kutoka katika albamu hiyo ni "AM to PM" na "When You Look at Me".

Nyimbo zote mbili zilipata kushika nafasi ya tatu katika chati bora za muziki wa Ufalme wa Muungano, lakini albamu yake haijapata kuuza nakala nyingi. Albamu ya pili ya Milian ni It's About Time, nayo haijafanikiwa kimauzo, lakini ilipokea Tuzo ya Grammy ikiwa kama albamu bora ya muziki wa R&B.

Wimbo maarufu kutoka katika albamu hiyo ni "Dip It Low", imekuwa nyimbo ya kwanza kwa umaarufu na kutunukiwa na Recording Industry Association of America kuwa kama wimbo bora kwa mauzo ya mtandaoni.

Remove ads

Muziki

Filamu

Maelezo zaidi Mwaka, Jina la filamu ...
Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads