Fuko-dhahabu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fuko-dhahabu
Remove ads

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Mafuko-dhahabu au mafuko butu ni wanyama wa familia Chrysochloridae ambao wanachimba katika ardhi na kushinda takriban maisha yao yote chini ya uso wake. Wanyama wengine waitwao fuko ni wanafamilia wa Bathyergidae na Spalacidae (oda Rodentia), Talpidae (Soricomorpha) na Notoryctidae (Notoryctemorphia). Spishi zote za fuko-dhahabu zinatokea Afrika kusini kwa Sahara. Hula wadudu. Mafuko hawa huchimba mahandaki yao na miguu ya mbele iliyo na ukucha wa tatu ambao umevuvumulika. Vidole vya kwanza na vya nne vimebaki kama masalio na kile cha tano kimepotea. Miguu ya nyuma ina vidole vitano vyenye ngozi katikati. Macho yao hayafanyi kazi na yamefunika kwa ngozi. Masikio ni vipenyo vidogo tu.

Remove ads

Hali ya sasa

Miongoni mwa spishi 21 za mafuko-dhahabu, angalau 11 zipo hatarini kwa kutoweka. Sababu za msingi ni uchimbaji wa mchanga, utendaji mbaya wa kilimo, ukuaji wa miji, na kuwindwa na mbwa na paka wa kufugwa.

Spishi

Remove ads

Picha

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads