Ciudad de la Paz

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ciudad de la Paz
Remove ads

Ciudad de la Paz (Kihispania: Mji wa Amani), [1] zamani iliitwa Oyala, ni mji katika Guinea ya Ikweta ambao unaendelea kujengwa kwenye mwaka 2022. Inakusudiwa kuchukua nafasi ya Malabo kama mji mkuu wa taifa. [2] [3]

Thumb
Tangazo la ujenzi wa daraja lililopangwa (2010)

Ilianzishwa kama eneo la mjini wa mkoa Wele-Nzas kwenye mwaka wa 2015.[4] Sasa ni makao makuu ya utawala ya mkoa mpya wa Djibloho ulioundwa mwaka wa 2017.[5] Mnamo 2017, mji huo ulipewa jina rasmi la Ciudad de la Paz ("Mji wa Amani"). [6] [7]

Mahali pa mji mpya palichaguliwa kwa ufikiaji wake mzuri na tabianchi. Kusudi muhimu ilikuwa kuunda mji mkuu kwenye eneo la bara, tofauti na mji mkuu wa sasa Malabo, ambao uko kwenye kisiwa cha Bioko .

Mji ulipangwa na kampuni ya usanifu ya Ureno. Unakusudiwa kuwa na takriban wakazi 200,000, [8] jengo jipya la bunge, ikulu ya rais na eneo la hekta 8150.

Ujenzi wa mji mkuu huu mpya umekosolewa na wapinzani wa kisiasa kwa Rais Teodoro Obiang aliyesukuma mpango huo. Serikali ya Guinea ya Ikweta ilianza kuhamia ofisi za kwanza tangu mwaka wa 2017. [9]

Remove ads

Mahali

Ciudad de la Paz iko karibu na katikati ya Río Muni ambayo ni sehemu ya kibara ya Guinea ya Ikweta. Iko kati ya miji ya Bata na Mongomo na 20 km kutoka uwanja wa ndege wa Mengomeyén . Ugavi wa umeme unategemea Bwawa la Djibloho linalozalisha megawati 120.[10]

Katikati ya msitu usio na maendeleo, serikali inapanga kujenga mji mpya kama makao ya serikali ya baadaye. [8] [11] Itakuwa makao makuu ya rais, serikali, utawala, polisi na uongozi wa kijeshi [11] na kuchukua nafasi ya mji mkuu wa sasa wa Malabo . Jiji linaundwa kuwa na makazi ya watu 160,000-200,000, wanaoishi katika eneo la 81.5 km 2 . Hii inalingana na takriban robo ya wakazi wa Guinea ya Ikweta.

Remove ads

Picha za miaka ya kwanza

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads