Conakry
mji mkuu wa Guinea From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Conakry (pia: Konakry) ni mji mkuu wa Guinea wenye wakazi 1,660,973 (mwaka 2014). Mji una bandari mwambaoni mwa Ghuba ya Guinea ya Atlantiki.



Historia
Chanzo cha Conakry ni kwenye kisiwa cha Tombo kilicho karibu sana na rasi ya Kaloum. Mji ulianzishwa baada ya kisiwa hicho kuhamishwa kutoka utawala wa Uingereza kwenda chini ya Ufaransa. Wafaransa waliunganisha mwaka 1887 vijiji vinne vya Conakry, Boulbinet, Krutown na Tombo. Mwaka 1889 Conakry ilikuwa makao makuu ya utawala wa koloni ya « Mito ya Kusini (Rivières du Sud) » na tangu 1891 ya Guinea ya Kifaransa ikakua kwa sababu ya bandari yake hasa baada ya kujengwa kwa reli kwenda Kankan.
Remove ads
Conakry leo
Leo kisiwa cha Tumbo kimeunganishwa na rasi ya Kaloum kwa barabara. Mji umeenea kufunika rasi yote. Kuna beledi tano mjini ambayo ni Kaloum (kitovu cha mji), Dixinn (penye chuo kikuu na balozi nyingi), Ratoma (penye vilabu na mabaa), Matam na Matoto penye uwanja wa ndege wa Gbessia.
Mahali pa kuangaliwa ni makumbusho ya kitaifa, masoko, jengo la Jumba la Watu, msikiti mkuu na visiwa vya Los.
Tazama pia
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Conakry kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads