Guinea
nchi huru katika Afrika Magharibi From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Guinea (pia: Gine, Gini; kwa Kifaransa: Guinée; kwa Kiingereza: Guinea; jina rasmi Jamhuri ya Guinea) ni nchi katika Afrika ya Magharibi. Pengine inatajwa kama Guinea-Conakry ili kuitofautisha na nchi za Guinea Bisau na Guinea ya Ikweta.
Imepakana na Guinea Bisau, Senegal na Mali upande wa kaskazini, Kodivaa, Liberia na Sierra Leone kusini halafu Bahari ya Atlantiki upande wa magharibi.
Eneo lake ni chanzo cha mito mikubwa ya Niger, Senegal na Gambia.
Remove ads
Jina
Jina la "Guinea" liliwahi kutaja sehemu kubwa ya Afrika ya Magharibi kati ya jangwa la Sahara na Ghuba ya Guinea ya Atlantiki likimaanisha "nchi ya watu weusi" kwa lugha ya Kiberberi.
Watu
Idadi ya wakazi ni milioni 14 hivi. Makabila yaliyopo nchini ni 24. Kubwa zaidi ni lile la Wafulani (40%).
Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wakazi wanatumia zaidi lugha asilia kadiri ya makabila, hasa Kipular, Kimandinka, Kisusu, Kikisi, Kikpelle na Kiloma,
Upande wa dini, 85% ni Waislamu (hasa Wasuni), 8% ni Wakristo (hasa Wakatoliki) na 7% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika.
Picha
Tazama pia
Viungo vya nje
Serikali
- Serikali ya Guinea Ilihifadhiwa 6 Januari 2010 kwenye Wayback Machine. (Kifaransa)
- Permanent UN Mission of the Republic of Guinea Ilihifadhiwa 17 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine. (Kifaransa)
Habari
- CIA World Factbook - Guinea Ilihifadhiwa 15 Juni 2006 kwenye Wayback Machine. (Kiingereza)
- BBC News Country Profile - Guinea (Kiingereza)
Muziki
- Cora Connection Ilihifadhiwa 10 Oktoba 1999 kwenye Wayback Machine. West African music resources (Kiingereza)
Orodha
- Open Directory Project - Guinea Ilihifadhiwa 25 Desemba 2005 kwenye Wayback Machine. directory category (Kiingereza)
- Stanford University - Africa South of the Sahara: Guinea directory category (Kiingereza)
- The Index on Africa - Guinea Ilihifadhiwa 24 Agosti 2004 kwenye Wayback Machine. directory category (Kiingereza)
- University of Pennsylvania - African Studies Center: Guinea directory category (Kiingereza)
- Yahoo! - Guinea Ilihifadhiwa 12 Machi 2007 kwenye Wayback Machine. directory category (Kiingereza)
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guinea kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads

