Nadharia ya njama
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nadharia ya njama (kwa Kiingereza: conspiration theory) ni masimulizi yanayodai kwamba kundi la watu ("wala njama") wamepatana kwa siri ("kula njama") kufanya mambo haramu au mabaya na kuyaficha mbele ya umma.

Nadharia za njama kwa kawaida zina ushahidi mdogo au zinakosa ushahidi wowote. Kuna pia nadharia za njama zinazorejelea matukio halisi lakini kuzieleza kutokana na njama isiyojulikana na watu wengi.
Nadharia nyingi za njama zinadai kwamba matukio fulani ya kihistoria hayakutokea jinsi yanavyoelezwa katika vitabu vya historia bali kufuatana na njama fulani.
Remove ads
Mifano
Nadharia za njama zilizokuwa maarufu katika miaka iliyopita ni pamoja na
- kwamba kutua mwezini kwa Apollo 11 hakukutokea[1], picha zote zilipigwa duniani tu[2]
- Shambulio la 11 Septemba 2001 lilitekelezwa na serikali ya Marekani ili kupata sababu ya kufanya vita katika nchi za Waislamu [3]
- rais John F. Kennedy wa Marekani aliuawa na polisi yake ya siri
- Wamasoni wana mpango wa kutawala dunia yote[4]
Remove ads
Nadharia za njama zilizosababisha majanga
Wakati nadharia za njama zilipolengwa dhidi ya kundi fulani katika jamii ziliweza kusababisha majanga kama mauaji ya kimbari au ya kidini.
- Mashtaka kuwa Wayahudi wa Ulaya walisababisha vifo vya miaka ya tauni kwa kutia sumu kwenye visima vilisababisha mashambulio dhidi ya jumuiya za Wayahudi na maelfu ya vifo
- Mashtaka dhidi ya Waarmenia kuwa walitaka kubomoa milki ya Osmani yalikuwa msingi kwa Maangamizi ya Waarmenia ya miaka 1915-1918
- Mashtaka dhidi ya Wayahudi wa karne za 19 na 20 kuwa walilenga kutawala Dunia waliweka msingi kwa itikadi ya Adolf Hitler na maangamizi makuu dhidi ya Wayahudi wa Ulaya
- Ubaguzi wa Wabahai nchini Iran umehalalishwa kwa imani kuwa hao ni mawakala wa polisi za siri za Uingereza, Marekani au Israeli.
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads