Dabarani

From Wikipedia, the free encyclopedia

Dabarani
Remove ads

Dabarani (ing. na lat. Aldebaran pia α Alpha Tauri, kifupi Alpha Tau, α Tau) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Tauri (Taurus). Ni pia nyota angavu ya 14 kwenye anga ya usiku. Mwangaza unaoonekana unacheza kati ya mag 0.75 na 0.95.

Thumb
Dabarani (Aldebaran) katika kundinyota lake la jinsi Ng’ombe (zamani Tauri, lat. Taurus) kwa mtazamaji wa Afrika ya Mashariki
Thumb
Ulinganifu wa ukubwa baina ya Aldebaran (Dabarani) na Jua; hata hivyo masi halisi ya Dabarani inafanana na Jua
Remove ads

Jina

Dabarani ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [1]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema الدبران al-dabaran ambalo linamaanisha “anayefuata”[2] kwa sababu inafuata nyota za Kilimia katika mwendo wa anga. Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulifuata desturi ya Kiarabu na kuorodhesha nyot hii kwa jina la "Aldebaran"[3].

Remove ads

Tabia

Dabarani - Aldebaran ina mwangaza unaoonekana wa Vmag 0.86 na mwangaza halisi ni -0.64. Hivyo no nyota angavu ya 14 kwenye anga ya usiku. Mwangaza wake unacheza kati ya 0.75 na 0.95.

Dabarani ni nyota ya karibu kiasi ikiwa umbali wake na Dunia ni miakanuru 65 -66 [4] . Masi yake ni M☉ 1.5- na nusukipenyo chake R☉ 45 (vizio vya kulinganisha na Jua letu) [5].

Ni nyota jitu jekundu katika kundi la spektra K5 III. Ilhali masi yake ni kidogo tu kubwa kuliko Jua letu kipenyo chake ni kubwa zaidi mara 45 na sababu yake ni ya kwamba jitu jekundu ni nyota iliyopanuka baada ya kuishiwa haidrojeni katika kitovu chake; katika hali hii kitovu cha nyota kinajikaza na myeyungano wa haidrojeni unahamia kwenye tabaka za nje za nyota. Hii inasababisha kupanuka kwa nyota na kuongezeka kwa mwangaza wake.

Remove ads

Tanbihi

Viungo vya Nje

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads