Ekuador

ni nchi kwenye pwani ya magharibi ya Amerika Kusini From Wikipedia, the free encyclopedia

Ekuador
Remove ads

Ekuador (kwa Kiswahili pia: Ekwado) ni nchi kwenye pwani ya magharibi ya Amerika Kusini.

Ukweli wa haraka


Thumb
Ramani ya Ekuador

Jina la nchi kwa Kihispania (Ecuador) lamaanisha "ikweta", na sababu ni kwamba imekatwa nayo.

Imepakana na Kolombia, Peru na Bahari ya Pasifiki.

Funguvisiwa la Galapagos (Archipiélago de Colón) ni sehemu ya Ekuador ikiwa na umbali wa karibu kilomita 1,000 kutoka bara.

Mji mkuu ni Quito, lakini mji mkubwa zaidi ni Guayaquil.

Remove ads

Watu

Wananchi wengi (71%) wana mchanganyiko wa damu ya Kizungu na ya Kiindio. Wenye asili ya Afrika ni 7.2%, Waindio ni 7%, na Wazungu ni 6.1%.

Ekuador ilikuwa koloni la Hispania, hivyo lugha ya wakazi wengi na lugha rasmi imekuwa Kihispania hadi leo. Lakini kuna Waindio wengi, hasa katika milima ya Andes, wanaoendelea kutumia lugha zao.

Asilimia 91.95 wana dini, na kati yao 80.44% ni Wakatoliki ma 11.3% Waprotestanti.

Remove ads

Tazama pia

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads