Eleazari mfiadini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Eleazari mfiadini (karne ya 3 KK - karne ya 2 KK) alikuwa mzee Myahudi aliyekubali kuuawa katika dhuluma ya mfalme Antioko Epifane kuliko kula nyama haramu au kudanganya kama kwamba ameila.

Akipendelea hivyo kifo kitukufu kuliko maisha ya aibu, alitangulia kishujaa wengine kwenda mahali pa mateso na kuacha mfano mzuri ajabu wa uadilifu[1][2].
Habari zake zinasimuliwa katika kitabu cha pili cha Wamakabayo, sura ya 6.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads