Helier Mtakatifu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Helier Mtakatifu (alifariki 555) alikuwa mkaapweke anaheshimika kama mmisionari wa kisiwa cha Jersey, karibu na Ufaransa[1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana tarehe 16 Julai[2].
Maisha

Mtoto wa wazazi tajiri wa Tongeren (leo nchini Ubelgiji). Ingawa Wapagani walikubali mtoto alelewe Kikristo, ila walipomuua Kunibert, mlezi wake, Helier alitoroka nyumbani.
Hatimaye alifikia Cotentin alipojiunga na monasteri ya Marcouf huko Nantus (Nanteuil, sasa St.-Marcouf-de-l’Isle, Manche).
Ni Marcouf aliyempeleka pamoja na padri Romard kuinjilisha Jersey ambapo hatimaye aliuawa na maharamia kwa kukatwa kichwa[3].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
