Monasteri

From Wikipedia, the free encyclopedia

Monasteri
Remove ads
Remove ads

Monasteri (kutoka Kiingereza "monastery") katika Ukristo ni jengo au majengo ya pamoja ambapo inaishi jumuia ya wamonaki, chini ya mamlaka ya abati. Kila moja inaweza kujitegemea, ingawa pengine yameundwa mashirikisho ili kusaidiana na kuratibu malezi na masuala mengine ya pamoja.

Thumb
Monasteri iliyoanzishwa na Mar Mattai aliyekimbilia Amid (Mesopotamia) wakati wa dhuluma za kaisari Juliano Mwasi (363).
Thumb
Monasteri ya Sumela, kusini kwa Trabzon, Uturuki, ilijengwa katika karne ya 4 (labda 386).
Thumb
Monasteri ya Mt. Katerina wa Aleksandria juu ya Mlima Sinai, mwanzo wa karne ya 6.
Thumb
Monasteri ya Bikira Maria huko El Paular, karibu na Madrid, Hispania.
Thumb
Monasteri ya Mt. Nilus katika kisiwa Stolbnyi kwenye Ziwa Seliger karibu na Ostashkov, Russia, 1910 hivi.

Monasteri ni tofauti na konventi, zilizoanzishwa na mashirika ya ombaomba, ambayo wanajumuia wake si wamonaki bali wanaitwa "ndugu".

Monasteri za Kikristo zilianza kujengwa baada ya kwisha kwa dhuluma za Dola la Roma dhidi ya Ukristo, ingawa hata kabla ya hapo kulikuwa na waamini wanaoishi namna fulani ya maisha ya kitawa.

Kwa karne nyingi monasteri zilikuwa kama mji mdogo unaojitegemea kiuchumi pia kutokana na mkazo uliowekwa katika kusali na kufanya kazi.

Kuna monasteri hata katika ya baadhi ya dini nyingine, hasa Ubuddha.

Remove ads

Tanbihi

Loading content...

Viungo vya nje

Loading content...
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads