Elhanan bin Jair
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Elhanan bin Jair (kwa Kiebrania אלחנן בן יערי) alikuwa mtu wa Bethlehemu kwenye mwaka 1000 KK.
Anatajwa na Kitabu cha Pili cha Samueli 21:19 kama muuaji wa jitu Goliathi, Mfilisti wa mji wa Gath[1][2].
Hata hivyo Kitabu cha Kwanza cha Samueli sura ya 17 kinasema kijana Daudi ndiye aliyeshindana na Goliathi akitumia kombeo na mawe akafaulu kumshinda na kumuua. Tofauti hiyo inatokana na jinsi vitabu hivyo viwili vilivyotungwa kwa kukusanya mapokeo yoyote juu ya mwanzo wa Ufalme wa Israeli bila kuyachambua[3].
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads