Emily Blunt

From Wikipedia, the free encyclopedia

Emily Blunt
Remove ads

Emily Olivia Laura Blunt (alizaliwa tarehe 23 Februari 1983) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Uingereza. Amejipatia tuzo kadhaa, ikiwa ni pamoja na Tuzo ya Golden Globe na Tuzo mbili za Screen Actors Guild, pamoja na uteuzi wa Tuzo ya Academy na Tuzo nne za British Academy Film. Mnamo mwaka wa 2020, jarida la Forbes lilimtaja kama mmoja wa waigizaji wa kike waliolipwa zaidi duniani.

Thumb
Emily mnamo 2019.

Blunt alianza kazi yake ya uigizaji kwenye jukwaa mwaka 2001 katika tamthilia ya The Royal Family na akamwigiza Catherine Howard kwenye mfululizo mfupi wa televisheni Henry VIII (2003). Alicheza kwa mara ya kwanza katika filamu mwaka 2004 kupitia My Summer of Love. Mafanikio yake yalijidhihirisha mwaka 2006 aliposhiriki kama mhusika mkuu katika filamu ya televisheni Gideon's Daughter na filamu ya vichekesho The Devil Wears Prada. Filamu ya kwanza ilimletea Tuzo ya Golden Globe kama Mwigizaji Msaidizi Bora. Umaarufu wake uliendelea kukua kupitia filamu kama The Young Victoria (2009), Salmon Fishing in the Yemen (2011), The Adjustment Bureau (2011), Looper (2012), Edge of Tomorrow (2014), na Into the Woods (2014).

Blunt alipata pongezi kubwa kwa uigizaji wake kama kachero wa FBI mwenye maadili katika filamu ya uhalifu Sicario (2015), kama mlevi katika filamu ya kusisimua The Girl on the Train (2016), na kama mama aliyeponyeka katika filamu ya kutisha ya mume wake John Krasinski, A Quiet Place (2018), ambayo ilimletea Tuzo ya SAG kama Mwigizaji Msaidizi Bora. Baadaye ameshiriki katika filamu zinazofuata Mary Poppins Returns (2018) na A Quiet Place Part II (2021), pamoja na mfululizo mfupi wa The English (2022). Uigizaji wake kama Katherine Oppenheimer kwenye filamu ya Christopher Nolan, Oppenheimer (2023), ulimletea uteuzi wa Tuzo ya Academy kama Mwigizaji Msaidizi Bora.

Tangu mwaka 2006, Blunt amekuwa akifanya kazi na Taasisi ya Marekani ya Kigugumizi kusaidia watoto kuondokana na tatizo hilo kupitia rasilimali za kielimu na kuongeza uelewa wa hali hiyo. Yupo kwenye bodi ya wakurugenzi ya taasisi hiyo, na pia huandaa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ufadhili wa masomo ya matibabu ya usemi kwa watoto na watu wazima.

Remove ads

Filmografia

Maelezo zaidi Namba, Jina la Filamu ...
Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads