Eneo la ng'ambo la Uingereza
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Eneo la ng'ambo la Uingereza ni lolote kati ya maeneo 14 ambayo ni chini ya serikali ya Uingereza lakini si sehemu za nchi.

(Eneo la Kiingereza kwenye Antaktika na Akrotiri na Dhekelia (Kupro) havionyeshwi)
Kwa Kiingereza yameitwa "British Overseas Territory" tangu ilipotungwa sheria ya mwaka 2002 badala ya jina la awali "British dependent territory" yalivyoitwa tangu mwaka 1981. Kabla ya 1981 yaliitwa "makoloni"
Hali ya maeneo hayo ni tofauti na ile ya Jumuiya ya Madola ambayo ni jumuiya ya hiari ya baadhi ya makoloni ya zamani ya Uingereza na nchi nyingine zilizopenda kujiunga.
Remove ads
Mambo ya kisheria
Kwa jumla wakazi wa maeneo ya ng'ambo ya Uingereza ni raia wa Uingereza na wana haki kuhamia Uingereza yenyewe. Kila eneo lina bunge lake na uhuru fulani wa kutunga sheria zake.
Visiwa vya mfereji wa Kiingereza (Jersey, Guernsey) na Isle of Man si maeneo ya ng'ambo ya Uingereza bali "maeneo chini ya taji la Uingereza".
Maeneo ya ng'ambo ya Uingereza
Remove ads
Viungo vya Nje
- Foreign and Commonwealth Office- "UK Overseas Territories"
- The Commonwealth - UK government site
- Decolonisation - History links for the end of the European formal Empires, casahistoria.net
- UK Overseas Territories Conservation Forum
- British Overseas Territories Act 2002- Text of the Act
- United Kingdom Overseas Territories Association
- Britlink - The British Overseas Territories
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads