Euplo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Euplo
Remove ads

Euplo (alifariki Catania, Italia, 12 Agosti 304) alikuwa shemasi aliyefia Ukristo kwa kukatwa kichwa wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian[1].

Thumb
Mchoro wa ukutani wa Mt Euplo, Melnik, Bulgaria, karne ya 12 au 13.

Kadiri ya mapokeo, gavana Kalvisiani alimtia gerezani kwa sababu alikutwa na Injili mikononi. Kisha kuhojiwa mara kadhaa, alipigwa hadi kufa kwa kuwa alijibu kwamba anajivunia kutunza Injili moyoni.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini, hasa tarehe 12 Agosti ambayo ndiyo sikukuu yake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads