Bulgaria
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bulgaria (kwa Kibulgaria: България;), rasmi kama Jamhuri ya Bulgaria, ni nchi katika Ulaya ya Kusini-Mashariki, iliyoko kwenye Rasi ya Balkan. Inapakana na Romania kaskazini, Serbia na Kisiwa cha Kaskazini-Mashariki magharibi, Macedonia Kaskazini kusini-magharibi, Ugiriki na Uturuki kusini, na Bahari Nyeusi mashariki. Ina idadi ya watu takriban milioni 6.4, ikiwa ya 108 duniani. Jiji lake kubwa zaidi na mji mkuu ni Sofia. Bulgaria imegawanyika katika mikoa 28. Inajulikana kwa historia yake tajiri iliyoanzia enzi za Thrakia, utamaduni wake wa Kislaviki, maeneo ya kihistoria kama Rila Monastery, na utalii wake wa milima na fukwe za Bahari Nyeusi.
Remove ads
Historia
Zamadamu walikuweko walau miaka milioni 1.4 iliyopita.
Kufikia mwaka 5000 hivi KK kulikuwa na ustaarabu mkubwa uliotengeneza vyombo vya ufinyanzi na usonara vilivyo kati ya vile vya awali zaidi duniani.
Baada ya mwaka 3000 KK, Wathraki walijitokeza katika rasi ya Balkani.
Mwishoni mwa karne ya 6 KK sehemu kubwa ya eneo hilo lilitekwa na Dola la Persia.
Katika miaka ya 470 KK, Wathraki waliunda ufalme wa Odrusia, ambao baadaye ulianguka na wenyewe walitawaliwa na Wamakedonia, Wakelti na Warumi. Mchanganyiko huo wa watu ulikuja kuungana na Waslavi, waliolowea rasi kwa namna ya kudumu baada ya mwaka 500 BK.
Mwaka 632 Wabulgaria walianzisha nchi huru kaskazini kwa Bahari Nyeusi iliyoitwa Bulgaria Kuu chini ya Kubrat hadi nusu ya pili ya karne ya 7.
Asparukh, mwandamizi wake, alihamia karibu na delta ya mto Danube akazidi kuteka maeneo ya Balkani yaliyokuwa ya Dola la Bisanti, jambo lililoendelea katika karne zilizofuata.
Huo mchanganyiko mkubwa wa watu ulipata utambulisho wa kitaifa kwa kushika dini, lugha na alfabeti moja.
Katika karne ya 11 hilo dola la Bulgaria la kwanza lilishindwa na Dola la Roma Mashariki likisaidiwa na Warusi.
Lakini mwaka 1185 ndugu Asen na Peter walifaulu kuanzisha dola la pili la Bulgaria lililofikia kilele chake katika miaka ya 1230.
Baada ya kugawanyika, falme tatu za Kibulgaria zilitekwa na Dola la Osmani mwaka 1396 kwa miaka 500 iliyofuata.
Vita kati ya Urusi na Uturuki vya miaka 1877–1878 vilileta uhuru kwa sehemu ndogo ya Bulgaria. Kwa kutaka Wabulgaria wote wawe ndani yake, nchi iliunga mkono Ujerumani katika vita vikuu vyote viwili na hatimaye ilishindwa.
Hivyo Bulgaria ikawa chini ya Wakomunisti kwa miaka 45.
Baada ya hapo Bulgaria ilijiunga na NATO mwaka 2004 na Umoja wa Ulaya mwaka 2007.
Remove ads
Watu
Wakazi wanazidi kupungua tangu mwanzo wa miaka ya 1990.
Wengi wao (84.8%) wanazungumza Kibulgaria, ambacho ni kati ya lugha za Kislavoni, na wanafuata dini ya Ukristo katika Kanisa la kitaifa ambalo ni kati ya Makanisa ya Kiorthodoksi.
Pia kuna makundi makubwamakubwa ya Waturuki (8.8%) Waislamu na walowezi kutoka India (4.9%).
Kwa jumla, Wakristo ni 75%, Waislamu 10%, wenye dini nyingine ni 3%, wakati wasio na dini ni 11.8%.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads