Eutimi abati

From Wikipedia, the free encyclopedia

Eutimi abati
Remove ads

Eutimi abati (pia: Eutimi mkuu; Melitene, Armenia, leo nchini Uturuki, 377[1][2] - 20 Januari 473) alikuwa mmonaki tangu utotoni, halafu padri na hatimaye abati nchini Palestina, alipokwenda kwa siri akiwa na umri wa miaka 30.

Thumb
Picha takatifu ya Mt. Eutimi.

Hadi kifo chake alikuwa na unyenyekevu na upendo mkubwa, pamoja na kufuata nidhamu [3]. Kutokana na umaarufu wake, alihamahama sehemu mbalimbali za nchi hiyo ili kukwepa umati uliomtafuta upwekeni[4][5][6][7].

Alipinga uzushi wa Eutike uliolaaniwa na mtaguso wa Kalsedonia (451) akafanya wamonaki wengi na hata malkia wamfuate katika imani sahihi.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Januari [8].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads