Palestina

From Wikipedia, the free encyclopedia

Palestina
Remove ads

Palestina (kwa Kiarabu: فلسطين‎ filasṭīn, falasṭīn; kutoka Kilatini: Palaestina; kwa Kiebrania: פלשתינה Palestina), rasmi kama Dola la Palestina, ni nchi katika Mashariki ya Kati, inayojumuisha maeneo mawili makuu: Ukingo wa Magharibi na Gaza. Ukingo wa Magharibi unapakana na Israeli upande wa magharibi na kaskazini, na Yordani upande wa mashariki, huku Ukanda wa Gaza unapakana na Israeli upande wa mashariki na kaskazini, na Misri upande wa kusini-magharibi. Nchi ina idadi ya watu takriban milioni 5.2, ikiwa ya 121 duniani. Mji wake mkubwa zaidi na wa kiutawala ni Ramallah, huku Yerusalemu ya Mashariki ikidaiwa kama mji mkuu rasmi. Palestina imegawanyika katika mikoa mbalimbali. Inajulikana kwa historia yake ya kipekee ya kidini, maeneo matakatifu ya dini kuu tatu, na harakati za kitaifa kwa uhuru wa kisiasa.[1]

Ukweli wa haraka Dola la Palestina دولة فلسطين (Dawlat Filasṭīn), Mji mkuu na mkubwa ...
Remove ads

Ramani na Matunzio

Thumb
Ramani ya maeneo yanayotazamiwa kuwa chini ya Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina
Thumb
Thumb
Thumb
Thumb
Yerusalemu kutoka Mlima wa Mizeituni
Thumb
Thumb
Thumb
Thumb
Thumb
Palestina 1759
Thumb
Palestina 1851
Thumb
Palestina 1864
Thumb
Palestina 1900
Thumb
Palestina 1915
Thumb
Palestine 1920
Thumb
Palestina 1924
Thumb
Palestina 1946
Thumb
Palestina 1947

Palestina (kwa Kiarabu: فلسطين‎ filasṭīn, falasṭīn; kutoka Kilatini: Palaestina; kwa Kiebrania: פלשתינה Palestina) ni jina la eneo lililoko upande wa Mashariki wa Bahari ya Mediteranea kati ya mkingo wa bahari hiyo na mto Yordani.

Remove ads

Historia ya jina na eneo la Palestina hadi 1948

Asili ya jina ilikuwa nchi ya Wafilisti iliyokuwa kanda nyembamba ya ardhi karibu na pwani ya bahari. Waroma wa kale walitumia jina hilo kwa jumla ya jimbo lao katika sehemu hizi.

Baada ya uvamizi wa Waarabu Waislamu jina liliendelea kutumiwa kwa umbo la Kiarabu "Filastin" na kutazamwa kama sehemu ya Shamu au Syria.

Tangu mwaka 1516 eneo lilitawaliwa na Milki ya Osmani. Kwa muda mrefu maeneo ya Palestina yalikuwa sehemu ya kusini ya jimbo la Dameski, na katika karne ya 19 jimbo la pekee la Yerusalemu liliundwa.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Uingereza ulitawala eneo hili kama eneo la kukabidhiwa la Shirikisho la Mataifa, na eneo hili lilikuwa pamoja na sehemu kubwa upande wa mashariki wa mto Yordani. Waingereza waligawa eneo katika sehemu mbili upande wa magharibi (Palestina yenyewe) na upande wa mashariki wa mto Yordani uliokuwa baadaye milki ya Yordani.

Kwenye sehemu ya magharibi iliyokuwa Palestina yenyewe kulikuwa na uhamiaji wa Wayahudi kutoka nchi za Ulaya ulioweka msingi kwa mapambano kati ya Israeli na Palestina ya baadaye.

Mwaka 1947 Umoja wa Mataifa uliamua kugawa Palestina katika sehemu tatu zilizopangwa kama Dola la Kiyahudi, Dola la Kiarabu na Yerusalemu kama mji wa kimataifa. Lakini Wayahudi walitangaza uhuru wa Dola la Israeli. Wenyeji Waarabu walipinga azimio hili na vita ilitokea. Baada ya mkataba wa kusalimisha amri Israeli mpya ilikuwa na sehemu ya Palestina kubwa kuliko awali. Asilimia kubwa ya wakazi Waarabu wa sehemu zilizokuwa chini ya Israeli mpya walikimbia au walifukuzwa nje. Ukanda wa Gaza ulishikwa na Misri na Ukingo wa Magharibi wa Yordani ulitawaliwa na milki ya Yordani.

Remove ads

Mapigano ya Wapalestina

Kati ya wakimbizi Waarabu waliokaa katika makambi huko Lebanoni, Syria, Yordani na Gaza kulikuwa na harakati ya kujielewa kama taifa la Wapalestina wakaunda vyama mbalimbali vya kupigania kurudi kwao lakini hii ilishindikana. Baada ya Vita ya siku 6 mwaka 1967 Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Yordani zilitwaliwa na jeshi la Israeli.

Harakati ya Wapalestina Waarabu iliendelea kupigania uhuru. Mapigano haya yalipata namna ya usuluhisho kwa muda na katika mapatano ya Oslo mwaka 1993 yalianzishwa Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina yaliyotangaza Dola la Palestina.

Palestina mpya

Kwa sasa Palestina ni nchi katika mwendo wa kupata uhuru kamili lakini hakuna uhakika mwendo huu utakamilishwa lini.

Maeneo ya Palestina yanatengwa kati ya sehemu chini ya serikali ya Palestina na maeneo yanayosimamiwa na Israeli.

Maeneo haya yako kati ya mto Yordani na pwani ya Mediteranea: ni hasa Ukingo wa Magharibi wa Yordani na Ukanda wa Gaza.

Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina ina kiwango fulani cha madaraka ya kiserikali katika baadhi ya maeneo haya.

Mamlaka hayo hutambuliwa na nchi nyingi za Waarabu kama serikali halisi. Jumuia ya kimataifa kwa ujumla imetambua mamlaka kwa viwango mbalimbali lakini si kama serikali kamili ya nchi huru. Hivyo Mamlaka ina kiti cha mtazamaji kwenye Umoja wa Mataifa.

Maeneo ya Palestina ya sasa yamepakana na Israeli, Yordani na Misri. Kanda la Gaza lina pwani kwenye Mediteranea.

Remove ads

Ramani za mabadiliko ya mipaka ya Palestina

Remove ads

Tazama pia

Viungo vya nje

Serikali

Israeli na Mamlaka ya Palestina

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads