Evangeline Lilly
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nicole Evangeline Lilly (amezaliwa Agost 3, 1979) ni mwigizaji wa kutoka Canada aliyepata umaarufu kutokana na kuigiza kwake kama Kate Austen kwenye kipindi cha Lost.
Maisha yake
Lilly alizaliwa mjini Fort Saskatchewan katika nchi ya Canada kutokana na familia ya Kikristo. Babake ni mwalimu, na mamake ni mtu wa mwanamitindo. Lilly ana dada wawili. Katika maisha yake ya utotoni, familia yao haikuwa na runinga.[1]
Uigizaji
Mwanzoni, Lilly alikuwa mwanamitindo. Alijiunga na Ford Models kama mwanamitindo, lakini akabadilisha mwenendo na kuwa mwigizaji wao.[2]
Mshahara wake wa Lost ni $80,000 kila kipindi. Kwa ajili ya Lost, alichaguliwa kama Breakout Stars of 2004 na Entertainment Weekly.Lilly amewekwa namba 13 kwenye orodha ya FHM "100 Sexiest Women in the World" mnamo 2006 na hapo awali alikuwa namba 2 kwenye orodha ya Maxim's "Hot 100" mnamo 2005.[3]
Remove ads
Maisha yake ya kibinafsi
Lilly alikuwa ameolewa na Murray Home, lakini wameachana.[4] Tangu 2004, amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji-mwenza wa Lost aitwaye Dominic Monaghan.
Mnamo 20 Desemba 2006, nyumba yake mjini Hawaii ilichomeka alipokuwa akirekodi Lost..[5] Chanzo cha moto huu ilisemekana kuwa ni hitilafu ya stima.
Tuzo
- Alichaguliwa kwa 2007 Golden Globe Award: Best Actress in a Drama lakini hakushinda.
- Alishinda tuzo la 2007 Screen Actors Guild Award: Outstanding Performance by Ensemble Cast in a Drama Series.
- Alichaguliwa kwa tuzo la 2005 Satellite Award: Best Actress in a Drama lakini hakushinda.
- Alichaguliwa kwa tuzo la 2006 National Television Award:Most Popular Actress lakini hakushinda.
- Hivi sasa, amechaguliwa kwa tuzo la 2010 Screen Actors Guild Award: Outstanding Performance by a Cast in a Motion Picture.
Remove ads
Filamu
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads