Remove ads

John David Jackson (amezaliwa tar. 18 Novemba 1977) ni msanii wa rekodi za hip hop kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Fabolous. Alikulia mjini Brooklyn huko New York City, alikuwa mmoja kati marapa wa pwani ya mashariki ambao waliathiriwa na muziki wa Southern hip hop. Moja kati ya kazi zake za awali ambayo ilimletea umaarufu ni pamoja na "Can't Deny It" mnamo 2001, kutoka katika albamu yake ya kwanza ya Ghetto Fabolous. Fabolous ametoa albamu tano, ambazo zote kwa ujumla zimeuza nakala zaidi ya milioni tatu huko nchini Marekani.[1]

Ukweli wa haraka Maelezo ya awali, Jina la kuzaliwa ...
Remove ads

Maisha na kazi

Maisha ya awali na mwanzo wa kazi

Fabolous alizaliwa John David Jackson mnamo tar. 18 Novemba 1977, na wazazi wenye asili ya Kiafrika-Kiamerika na Kidominika.[2][3] Alikulia huko Bedford-Stuyvesant jirani kidogo na Brooklyn, New York.[4][5] Wakati anasoma elimu ya juu, Fabolous akaanza kujifua katika masuala ya muziki wa rap. Alialikwa kurap moja kwa moja kipindi cha redio cha DJ Clue na kwenye WQHT Hot 97, ambapo kulimpatia uwezo wa kuweza kuingia mkataba na studio ya Desert Storm Records.[6] Alipata kushirikishwa kwenye mamixi tepu kibao ya DJ Clue na mamixi tepu mengine mingi tu ya wasaniii wa Roc-A-Fella.

Remove ads

Diskografia

Makala kuu: Diskografia ya Fabolous
  • Ghetto Fabolous (2001)
  • Street Dreams (2003)
  • Real Talk (2004)
  • From Nothin' to Somethin' (2007)
  • Loso's Way (2009)
  • Loso's Way 2 (2010)[7]

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads