Felisi wa Nicosia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Felisi wa Nicosia, O.F.M.Cap. (jina la awali Filippo Giacomo Amoroso) alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka Sicilia, leo nchini Italia (5 Novemba 1715 – 31 Mei 1787).

Baada ya kukataliwa miaka 10, alipopokewa utawani alitoa kwa unyofu na usafi wa moyo huduma duni alizoagizwa [1].
Ni maarufu hasa kwa utiifu wake wa ajabu, uliothibitishwa na kiongozi aliyejichukulia jukumu la kumjaribu na kumdhalilisha kwa kila namna.[2]
Papa Leo XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 12 Februari 1888, halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 23 Oktoba 2005.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads