Wakapuchini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wakapuchini ni watawa Wafransisko wa Kanisa Katoliki.
Idadi yao inakaribia wanaume 10,000 duniani kote, wakiongozwa na ndugu Roberto Genuin wa kanda ya Veneto. Ni shirika la kiume la nne kwa wingi wa watawa duniani.
Maana ya jina
Jina linatokana na neno la Kiitalia "cappuccio", lenye maana ya kikofia kilichoshonwa kwenye kanzu yao ya rangi ya kahawia.
Historia
Tawi hilo lilianzishwa na Mathayo wa Bascio pamoja na Ludoviko wa Fossombrone na Rafaeli wa Fossombrone mwaka 1525, ambao walilenga maisha ya kifukara kuliko yaliyofuatwa na Ndugu Wadogo wenzao.
Urekebisho huo, uliojitahidi sana kufuata kikamilifu kanuni ya Ndugu Wadogo na mifano ya mwanzilishi, Fransisko wa Asizi, ulipata kibali cha Papa Klementi VII mwaka 1528.
Baada ya hapo kutoka mkoa wa Marche shirika likaenea na kuzaa matunda mengi ya utakatifu kuanzia bradha Felix wa Cantalice hadi padri Pio wa Pietrelcina.
Bernardino wa Asti, aliyeshika uongozi miaka 1535-1538, ndiye aliyelipa shirika jipya sura ya kiroho ya kudumu, hasa kwa njia ya katiba iliyotungwa mwaka 1535 na kupitishwa mwaka uliofuata, halafu ikatumika hadi mwaka 1968 bila mabadiliko makubwa.
Remove ads
Takwimu
Mnamo tarehe 31 Desemba 2023, Wakapuchini duniani walikuwa 9,684, kati yao mapadri 6.819. Mwaka 2011 walikuwa katika nchi 106: Afrika 1321; Amerika ya Kilatini 1720; Amerika ya Kaskazini 662; Asia-Oceania 2283; Ulaya 4378.[1]
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads