Fermi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Fermi (Fermium) ni elementi sintetiki yenye alama Fm na namba atomia 100. Katika jedwali la elementi hupangwa katika kundi la aktinidi. Kati ya elementi sintetiki ni elementi nzito zaidi, inaweza kupatikana kwa njia ya kufyatulia nyutroni dhidi ya elementi nyepesi. Ni elementi ya kimetali ingawa metali safi ya Fermi haijatengenezwa bado. [1] Kwa jumla kuna isotopi zake 19 zinazojulikana, ikiwa 257Fm ni isotopi yenye nusumaisha ndefu zaidi iliyo na siku 100.5. Kwa sababu ya kiwango kidogo cha fermi iliyozalishwa na nusumaisha fupi ya isotopi zake zote, kwa sasa hakuna matumizi yoyote nje ya utafiti wa msingi wa kisayansi.
Fermi iligunduliwa katika taka ya mlipuko wa bomu la hidrojeni la kwanza mnamo 1952.[2] Ilipokea jina lake kwa kumbukumbu ya Enrico Fermi, mmoja wa waanzilishi wa fizikia ya nyuklia.


Remove ads
Marejeo
Kujisomea
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads