Filastri

From Wikipedia, the free encyclopedia

Filastri
Remove ads

Filastri (330 - 387 hivi) anakumbukwa kama askofu wa 6 wa Brescia (Italia Kaskazini)[1].

Thumb
Mchoro wa ukutani unaomuonyesha Mt. Filastri.

Asili yake haijulikani: zinatajwa Italia, Hispania na Misri.

Alitunga kitabu kilichoorodhesha aina 156 za uzushi (Diversarum Hereseon Liber; kifupi: De Haeresibus) kutokana na safari zake nyingi za kimisionari alipopigwa mijeledi pia.

Alisifiwa na mwandamizi wake Gaudioso wa Brescia katika hotuba ya kila mwaka; imetufikia moja, iliyo chanzo kikuu cha taarifa juu ya maisha na kifo chake[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Julai[3][4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Matoleo ya kitabu chake

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads