Fileas

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Fileas (alifariki Aleksandria, 311 hivi) alikuwa askofu wa Thmuis, Misri, ambaye, akikataa mashauri ya ndugu zake, alifia dini yake kwa kukatwa kichwa pamoja na wenzake 650 hivi wakati wa dhuluma ya makaisari Diokletian na Galerius[1][2].

Kati ya majina yao kuna akida Filoromus, maaskofu Pakomi, Theodori na Petro, halafu Fausto, Didius, Amoni, Hesiki na Viktorina[3].

Masimulizi ya kifodini chao yaliandikwa kwa Kigiriki miaka 15 baadaye na sehemu fulani imetufikia.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 4 Februari[4] au 26 Novemba.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads