Filipo Benizi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Filipo Benizi
Remove ads

Filipo Benizi, O.S.M. (Firenze, Italia ya Kati, 15 Agosti 1233 - Todi, Italia ya Kati, 23 Agosti 1285) alikuwa padri mtawa wa shirika la Watumishi wa Maria.

Thumb
Sanamu yake huko Padova.

Ingawa aliingia utawani abaki bradha, baadaye alipadrishwa akafikia kuwa mkuu wa shirika lote (1267) akalieneza kwa bidii [1].

Pamoja na hayo alikuwa maarufu kwa unyenyekevu wake na kumuona Yesu msulubiwa kuwa kitabu chake pekee [2]

Alitangazwa na Papa Inosenti X kuwa mwenye heri tarehe 8 Oktoba 1645, halafu Papa Klementi X alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Aprili 1671.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Agosti[3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads