Fonte Colombo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fonte Colombo
Remove ads

Fonte Colombo ni patakatifu pa Kanisa Katoliki karibu na Rieti, Italia ya Kati, maarufu kama mahali ambapo Fransisko wa Asizi alikamilisha kanuni ya Ndugu Wadogo katika majira ya baridi kati ya mwaka 1222 na 1223. Panapatikana kwenye kimo cha mita 549 juu ya usawa wa bahari.

Thumb
Kanisa lilivyo leo.
Thumb
Sanamu ya Mt. Fransisko huko Fonte Colombo.

Usuli

Kuanzia mwaka 1209 hadi mwaka 1921 Fransisko, kwa kushirikiana na wafuasi wake na uongozi wa Kanisa hilo alikuwa ameandika kanuni isiyothibitishwa, ambayo iliongoza utungaji wa kanuni ya kudumu. Kwa nini kanuni hiyo haikuthibitishwa? Nani hakuridhika nayo? Mwenyewe au wafuasi wake au viongozi wa Kanisa? Hakika yeye alipendezwa nayo sana kwa jinsi inavyohimiza kuishi Kiinjili: ndiyo sababu mwishoni aliandika ndugu hawaruhusiwi kuongeza wala kupunguza wala kubadili hiyo kanuni.

Kumbe Kanisa lilidai kanuni iwe na sura ya kisheria zaidi. Hivyo kazi ya Fransisko ikaendelea, alivyoshuhudia hasa ndugu Leo ambaye alikuwa karani wake na kufuatana naye na ndugu Bonisyo kwenye mlima wa Fonte Colombo. Leo ametueleza upinzani wa akina Elia Bombarone na uchungu wa Fransisko aliokuwa anautoa katika sala, hasa kutokana na hakika aliyokuwanayo juu ya matakwa ya Mungu kwa shirika lake: alikuwa akitulia tu katika nia yake ya kuzidi kuonyesha kwa matendo yake yale ambayo Yesu alimfunulia.

Hata hivyo, ndugu wengi hawakukubali kuyapokea kama sheria kwao. Ilimbidi akubali baadhi ya madai yao, pamoja na mashauri mbalimbali ya Kardinali mlinzi na labda ya Papa mwenyewe. Lakini, pamoja na kutimiza hivyo udogo wake, hakukubali kuacha yaangushwe mambo makuu ya wito wake. Hivyo kanuni ya kudumu kwa jumla inafuata ile isiyothibitishwa, tena inaonyesha wazi kuwa mwandishi mkuu ni Fransisko, pia mengine yamesisitizwa naye hata kuliko alivyofanya katika kanuni ya muda.

Hatimaye tarehe 29 Novemba 1223 kanuni ilithibitishwa na Papa Honori III ikawa sheria ya Kanisa ambayo Fransisko mwenyewe hakuweza kuibadilisha tena. Kwake na kwa Kanisa haukuwepo wasiwasi kuhusu kanuni kuwa ileile ingawa imerekebishwarekebishwa. Kama vile tangu mwaka 1209 hadi 1223, hata baadaye alidai kuwa ndiyo Injili yenyewe, yaani kiini chake.

Remove ads

Marejeo

  • L. Wadding, Annales Minorum, seu Trium Ordinum a S. Francisco institutorum, 1931
  • A. Terzi, Memorie francescane nella Valle Reatina, Rieti, Il Velino, 1955
  • Fonti Francescane. Editio Minor, Assisi, Movimento Francescano, 1986
  • a c. di M. Righetti Tosti Croce, La Sabina Medievale, Rieti, CARIRI, 1990
  • a c. di L. Pellegrini e S. da Campagnola, Il francescanesimo nella Valle Reatina, Rieti, CARIRI, 1993
  • G. Pampaloni, Francesco nella Valle Santa di Rieti, Rieti, EPT, 1995
  • Anonimo Reatino, Actus Beati Francisci in Valle Reatina, a c. di A. Cadderi, Assisi, Edizioni Porziuncola, 1999
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Fonte Colombo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads