Papa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Papa (kutoka neno la Kilatini lenye asili ya Kigiriki, πάππας, pappas,[1][2]) ni jina linalotumika kawaida kumtaja askofu wa Roma, kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, ambalo ndilo kubwa kabisa kati ya madhehebu ya Ukristo. Kama mwandamizi wa Mtakatifu Petro, mkuu wa Mitume kumi na wawili wa Yesu, anayeaminika kuongoza Kanisa la Roma hadi kifodini chake, Wakatoliki wanamchukulia Papa kuwa mwakilishi wa Kristo duniani, akiwa ishara inayoonekana ya umoja na mwenye mamlaka ya juu katika masuala ya mafundisho ya imani, maadili, na uongozi wa Kanisa.[3]
Kwa samaki anayeitwa kwa Kiswahili "papa", tazama papa (samaki).

Papa anaishi katika Mji wa Vatikani, dola huru lililozungukwa na mji wa Roma. Majukumu yake ni pamoja na kuteua maaskofu, kuongoza sinodi na mitaguso, kutoa nyaraka rasmi za Kanisa kama vile waraka (encyclicals) na mahimizo ya kitume (apostolic exhortations), na kuliongoza Kanisa duniani katika utume wake wa uinjilishaji na utoaji wa misaada ya upendo. Kwa karne nyingi, nafasi ya Papa imepanuka kujumuisha ushirikiano wa kidiplomasia na viongozi wa mataifa na kushiriki katika masuala mapana ya kijamii na kibinadamu, huku akiendelea kuwa nguzo ya imani kwa zaidi ya Wakatoliki bilioni moja duniani kote.
Remove ads
Asili
Kiasili neno la Kilatini "Papa" linamaanisha "Baba", nalo likawa cheo kutokana na nia ya kumtaja askofu wa Roma kwa heshima ya pekee. Msingi wa heshima hiyo ni imani ya Wakatoliki kuwa askofu wa Roma ni mwandamizi wa Petro, mkuu wa mitume wa Yesu.
Wakatoliki huamini ya kwamba Petro alipewa na Yesu kazi ya kuongoza Kanisa lote kwa niaba yake na ya kwamba jukumu hilo linaendelea kati ya waandamizi wa Petro kwenye kiti cha askofu wa Roma ambacho kwa heshima kinaitwa Ukulu mtakatifu.
Remove ads
Historia
Upapa ni kati ya vyeo vya zamani zaidi duniani na umeathiri sana historia ya binadamu kwa miaka karibu 2000.[4]Athari hiyo iliweza kuwa nzuri au mbaya, kadiri ya matendo ya mhusika.[5][6][7]
Kwa muda mrefu mamlaka ya Papa upande wa siasa, hasa juu ya mikoa ya Italia ya Kati, ilisababisha nchi nyingine na koo tajiri za Roma zijiingize katika uchaguzi ili kupitisha watu wao, hata wasiofaa. Upande mwingine, Mapapa waliathiriwa na utamaduni na mazingira ya nyakati zao, hasa tapo la Renaissance, kiasi cha kuzama katika anasa.
Baada ya Dola la Papa kutekwa na Ufalme wa Italia (1860-1870), Mapapa wameweza kushughulikia zaidi mambo ya kiroho na kujitokeza kwa ubora.[8][9]Kwa miaka ya karibuni inatosha kumfikiria Papa Yohane Paulo II na mchango wake katika kuangusha ukomunisti katika Ulaya Mashariki.
Remove ads
Majina ya mapapa

Papa huchaguliwa na makardinali wa Kanisa Katoliki baada ya mtangulizi wake kufa au kung'atuka. Baada ya kuchaguliwa papa mpya anaweza akajipatia jina jipya. Tangu tarehe 13 Machi 2013 ni Papa Fransisko, ambaye awali aliitwa Jorge Mario Bergoglio, kutoka Argentina.
Majina ya mapapa wengine wa Kanisa Katoliki yanapatikana katika orodha ya mapapa.
Mkuu wa Vatikano
Papa ni pia mkuu wa nchi huru ya Mji wa Vatikano iliyopo ndani ya mji wa Roma (ambao ni mji mkuu wa Italia).[10]
Cheo cha "Papa" penginepo
Cheo cha Papa hutumiwa pia na baadhi ya madhehebu mengine ya Kikristo kwa viongozi wao, hasa kwa mkuu wa Kanisa la Kikopti huko Misri.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads