Kardinali mlinzi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kardinali mlinzi
Remove ads

Kardinali mlinzi alikuwa kardinali aliyeteuliwa na nchi, mashirika ya kitawa, vyama vya kitume, makanisa, mabweni na miji au aliyetolewa na Papa kwa miundo hiyo ili aisimamie kwa niaba yake na kuitetea huko Roma katika ofisi kuu za Kanisa Katoliki.

Desturi hiyo ilianza katika karne ya 13 Fransisko wa Assisi alipomuomba papa Inosenti III na halafu papa Onori III apewe Ugolino, kardinali wa Ostia, kama mlinzi wa utawa wake wa Ndugu Wadogo.

Mamlaka ya kardinali mlinzi iliongezwa au kupunguzwa kadiri ya mang'amuzi mpaka iliposimamishwa kwa jumla baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano (1962-1965).

Thumb
Papa Gregori IX, rafiki wa Fransisko wa Assisi, kabla ya kuchaguliwa kuwa Papa, alikuwa Kardinali mlinzi wa kwanza.
Remove ads

Marejeo

  • HIERONYMI PLATI, Tractatus de cardinalis dignitate et officio (Rome, 1836), XXXIII
  • HUMPHREY, Urbis et Orbis (London, 1896).
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kardinali mlinzi kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads