Fosyo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fosyo
Remove ads

Fosyo (kwa Kigiriki: Φώτιος, Fōtios[1]; Konstantinopoli (leo nchini Uturuki), 810/820Bordi, Armenia, 6 Februari 893) alikuwa Patriarki wa Konstantinopoli miaka 858-867 halafu 877-886;[2] Kwa ujuzi wake mkubwa[3] na kwa umuhimu wake katika historia ya Kanisa, Waorthodoksi wanamuita Fosyo Mkuu[4].

Thumb
Picha takatifu ya Mt. Fosyo Mkuu katika ukuta wa kanisa kuu la Mt. Sofia, Kiev (Ukraina).

Farakano la muda la miaka 863-867 kati ya Kanisa la Roma na lile la Konstantinopoli kuhusu upatriarki wa Fosyo lilikuwa baya kuliko yote kabla ya farakano la mwaka 1054 ambalo limedumu hadi leo kati ya Ukristo wa Magharibi na Waorthodoksi.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi kwama mtakatifu[5], ingawa alitangazwa rasmi mwaka 1847 tu.

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads