Frances Cabrini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Fransiska Saviera Cabrini (Sant'Angelo Lodigiano, Italia, 15 Julai 1850 – Chicago, Illinois, Marekani, 22 Desemba 1917) alikuwa mwanzilishi wa shirika la Masista Wamisionari wa Moyo Mtakatifu (kwa Kiingereza Missionary Sisters of the Sacred Heart).
Jumuiya hiyo ilianzia Italia na kufanya kazi hasa Marekani kati ya wahamiaji kwa kujenga shule, hospitali na nyumba kwa watoto yatima kwa kufuata mfano wake aliyejitoa kwa kila namna kuhudumia wahamiaji kwa upendo mkubwa ajabu [1].
Mwaka 1946 Mama Cabrini alitangazwa kuwa mtakatifu akiwa raia Mmarekani wa kwanza kupewa heshima hiyo.
Sikukuu yake ni tarehe 22 Desemba[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads