Yatima

mtoto ambaye wazazi wake wamekufa au wamewaacha kabisa From Wikipedia, the free encyclopedia

Yatima
Remove ads

Yatima (kwa Kiingereza orphan, kutoka Kigiriki ορφανός, orfanós[1]) ni mtoto aliyefiwa au kutelekezwa moja kwa moja na wazazi wake wote[2][3]. Kwa kawaida mtoto aliyewapoteza wazazi wake wote wawili anaitwa yatima.

Thumb
Mayatima, mchoro wa Thomas Kennington.

Watu wazima pia wanaweza kuitwa mayatima. Ingawaje, watu waliofikia utu uzima kabla wazazi wao hawajafariki kwa kawaida hawaitwi hivyo.

Kwa ujumla hili ni neno ambalo hutumika kuelezea watoto ambao wazazi wao walifariki kabla ya wao kufikia umri wa kujitegemea.

Remove ads

Hali ya yatima

Watoto yatima mara nyingi huishi katika ukoo wa wazazi, katika nyumba ya yatima au kwa walezi. Katika nchi maskini pasipo mfumo mzuri wa nyumba za yatima kuna idadi kubwa ya mayatima wanaopaswa kuishi kwa kuombaomba au kutafuta riziki kwa kufanya kazi duni na hatari.

Kuasiliwa

Kama yatima anaasiliwa na walezi anakuwa mtoto wao kisheria[4] ingawa hali hii inaweza kuwa tofauti kulingana na sheria za nchi mbalimbali; hasa nchi nyingi za Kiislamu hazikubali mfumo wa kuasili kamili ila tu mfumo wa "kafala" ambayo ni aina ya ulezi ambapo mtoto anayepokelewa kisheria haitazamiwi kama mwanaukoo. [5]

Katika dini

Vitabu mbalimbali vya dini, vikiwemo vile vya Biblia[6] na Kurani[7] , vinasema sana kuhusu watoto yatima ili kutetea haki zao na kuhimiza huruma kwao. Muhammad mwenyewe alikuwa yatima.

Takwimu

Thumb
Msichana wa Afghanistan katika nyumba ya watoto yatima mjini Kabul mnamo Januari 2002.

Mayatima si wengi katika nchi zilizoendelea, lakini ni wengi katika nchi zinazoendelea au zenye vita.

Maelezo zaidi Bara, Idadi ya mayatima (mara elfu) ...
Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads