Fransisko Blanco
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fransisko Blanco alikuwa padri wa shirika la Ndugu Wadogo Pekupeku kutoka Hispania na mmisionari aliyefia dini Japani (+1597).

Dhuluma dhidi ya Wakatoliki zilipozidi, yeye na wenzake 25 (mapadri na watawa 8 na walei 17[1]) walikamatwa, walitukanwa na kuteswa vikali, na hatimaye wakasulubiwa huko Nagasaki tarehe 5 Februari mwaka 1597, huku wakifurahia neema ya kuuawa namna ileile ya Yesu [2].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake na ya wafiadini wenzake huadhimishwa kila mwaka tarehe 6 Februari[3].
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.